Taarifa ya kudhibiti nzi wa kwenye matunda wa Queensland (Managing Queensland fruit fly, Swahili)

Pakua: NZI wa kwenye matunda wa Queensland (PDF - 452.5 KB)

Nzi wa kwenye matunda wa Queensland anapatikana Victoria na hushambulia matunda mengi na mboga za majani. Kijarida hiki kitakusaidia kuangalia nzi wa kwenye matunda wa Queensland katika bustani yako na kulinda matunda na mboga za majani unazolima ili zisiharibiwe.

NZI wa kwenye matunda wa Queensland yukoje?

Nzi wa kwenye matunda wa Queensland ana hatua nne za kukua. Nzi anaweza kubadilika kutoka yai kwenda utu uzima ndani ya siku 30 katika hali nzuri ya hewa (k.m. 26 ⁰C).

Mayai

Buu

Pupa

Nzi Kamili

Nzi wa kwenye matunda wa Queensland anaweza kupatikana kwenye bustani wakati wa kipupwe, kiangazi na vuli.

VIMELEA VYA NZI WA MATUNDA WA QUEENSLAND MAARUFU VILIVYOKUZWA NYUMBANI

Nzi wa matunda wa Queensland hutaga mayai ndani ya matunda na mboga za majani mbalimbali – hivi huitwa vimelea’. Baadhi ya mifano yao inayojulikana imeonyeshwa hapa chini.

apple, parachichi, parachichi, capsicum, pilipili cumquat, mbilingani, mtini, zabibu, limau, chokaa loquat, nectarini, machungwa, matunda ya shauku, peach, peari, persimmon, plum, komamanga, peari ya kuchomoza, quince, jordgubbar, nyanya

Orodha kamili ya vimelea inapatikana kwenye www.agriculture.vic.gov.au/qff

KUDHIBITI NZI WA KWENYE MATUNDA WA QUEENSLAND KATIKA BUSTANI

1. Kwanza angalia nzi wa kwenye matunda wa Queensland

Mitego: Tazama kama nzi wa kwenye matunda wa Queensland yuko kwenye bustani yako kwa kuning'iniza mitego ya nzi wa kwenye matunda wa Queensland. Ning'iniza mitego kwenye wastani wa meta 1.5 juu kwenye kivuli kilicho karibu, mti mbichi kabisa. Anza hii wakati wa masika na kuendelea mpaka wakati kipupwe.

Kuna mitego mbalimbali ambayo inawavutia na kuwashika nzi wa kwenye matunda wa Queensland. Mitego hiyo pia inaweza kuwavutia na kuwashika wadudu wengine ambao ni wazuri kwa ajiri ya bustani yako, hivyo angalia kama umemkamata nzi wa kwenye matunda wa Queensland kabla ya kutumia dawa ya kuuwa wadudu kwenye mti au matunda yako.

2. Njia za kuzuia

Kama ukiona nzi wa kwenye matunda wa Queensland kwenye bustani yako, utaweza kudhibiti vizuri kwa kutumia njia mbalimbali za kuzuia. Anza njia za kuzuia kwa angalau wiki 6-8 kabla ya matunda kuiva yaweze kuchumwa kwa sababu nzi wa kwenye matunda wa Queensland wanaweza kutaga mayai ndani ya tunda la kijani na gumu

Kuyatenga ni kitu kizuri: Tumia mitego ya wadudu, vikapu na vifuniko kwa ajiri ya kufunika matunda baada ya kuwa yamerutubishwa ili kuzuia nzi wa kwenye matunda wa Queensland kuweza kutaga mayai ndani ya tunda au mboga za majani. Usiruhusu mitego iguse matunda.

Kuyatenga ni kitu kizuri: Tumia mitego ya wadudu, vikapu na vifuniko kwa ajiri ya kufunika matunda baada ya kuwa yamerutubishwa ili kuzuia nzi wa kwenye matunda wa Queensland kuweza kutaga mayai ndani ya tunda au mboga za majani. Usiruhusu mitego iguse matunda.

Dawa za wadudu, mitego na dawa za kupuliza: mitego na dawa ya nzi wa kwenye matunda ya Queensland hulinda na kushika nzi wa kwenye matunda kwenye bustani yako kabla ya kuvamia matunda. Tazama mitego ambayo itaua wadudu wote wa kike na kiume. Mitego peke yake haiwezi kudhibiti wadudu wa kwenye matunda.

Dawa za matunda zinapatikana pia ambazo zinaua mdudu wa nzi wa kwenye Queensland. Dawa za wadudu zinaweza kuua kama zikitumiwa vibaya - soma na fuata maelekezo ya kwenye kibandiko.

Aina zote hizi za bidhaa zinanunuliwa kwenye maduka ya mimea, maduka ya bustani za nyumbani na wachuuzi wa kwenye mitandao.

3. Tazama matunda na mboga za majani

Tazama alama za mchubuko kwenye ngozi/ganda na buu ndani ya matunda na mboga za majani.

Tazama alama za mchubuko kwenye ngozi/ganda na buu ndani ya matunda na mboga za majani.

4. Matunzo ya bustani ya mhimu (usafi mzuri)

Chagua na tumia tunda wakati limeiva. Toa matunda na mboga za majani zote ambayo yanakuwa yameoza, yameanguka chini na matunda ambayo hutaki kuyala. Hii itamzuia nzi wa kwenye matunda wa Queensland kuweza kuzaana katika bustani yako.

Safisha kwa kukatia miti ya matunda ili uweze kuifikia vizuri wakati wa kuchuma, kuweka nyavu za wadudu na kuweka dawa ya kupuliza.

Kabla ya kutupa tunda, unahitaji kuua buu lolote ambalo linaweza kuwa ndani kwa kuweka kwenye friza, microwevu, kuchemsha, au kwenye mwanga wa sola (kufungia matunda kwenye bagi la plastiki na kuliacha kwenye jua kwa mda wa siku 14). Baada ya kufanya hivi, matunda yaliyofungiwa kwenye bagi yanaweza kuwekwa kwenye pipa la takataka.

Usiweke mbolea kwenye matunda na mboga za majani ambazo zimeathiliwa au kuharibiwa na nzi wa kwenye matuda wa Queensland.

Kama huwezi kutunza miti ya matunda na mboga za majini, ibadilishe kwa miti isiyozoeleka, miti ya maua (k.v. mimea ya asili).

USIENEZE NZI WA KWENYE MATUNDA WA QUEENSLAND

Njia nzuri ya kusimamisha nzi wa kwenye matunda wa Queensland katika kuenea maeneo mapya ni kutokusafiri na matunda au mboga za majani zenye ugojwa na hasa zile zinazooteshwa majumbani

Adhabu zinaweza kutolewa kama ukigundulika kuwa unasafiri na mmea ambao umeathirika kwenda baadhi ya maeneo – kwa taarifa zaidi tembelea www.interstatequarantine.org.au.

Taarifa zaidi zinaweza kupatikana kwenye www.agriculture.vic.gov.au/qff au kwa kupiga simu Kituo cha Huduma kwa Mteja kwa 136 186.

Hii imedhibitishwa na kuchapishwa na Idara ya Kazi ya Viztoria, Precincts and Regions,1 Spring Street, Melbourne, March 2020

© Idara ya Kazi ya Mkoa wa Victoria, Precincts and Regions 2020

Page last updated: 21 Jun 2024